BENCHI la Ufundi la Azam FC chini ya kocha mkuu, Mcameroon Joseph Omog pamoja na wachezaji, wamemkaribisha kwa shangwe kiungo Amri Kiemba ambaye kwa mara ya kwanza alianza mazoezi na kikosi hicho jana Jumatatu.
Kiemba ambaye amesajiliwa kwa mkopo na Azam kwa
muda wa miezi sita akitokea Simba, alianza mazoezi hayo sambamba na
mchezaji mwingine mpya Muivory Coast, Sanaly Bamba ambaye ni kiungo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Omog alisema:
“Nimefurahi kuona Kiemba tupo naye kwenye timu, ndiyo ameanza mazoezi
leo lakini namjua ni mchezaji mzuri nimemfuatilia kwa kipindi kirefu.
“Nilimwona pia kwenye mechi ya Taifa Stars waliyocheza na Benin ni mzuri, ukweli najivunia kuwa naye.”
Kwa upande wa wachezaji, nahodha msaidizi wa Azam,
Himid Mao alisema: “Kiemba ni mchezaji mzuri kila mtu anajua na hiyo
ndiyo sababu viongozi wakamleta kwenye timu.
“Ninachoweza kusema, kama wachezaji tutampa ushirikiano mzuri tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya timu.
“Ninachoweza kusema, kama wachezaji tutampa ushirikiano mzuri tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya timu.
Katika mazoezi hayo hawakuwapo wachezaji walio
katika timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’. Hao ni Mwadini Ally,
Abdallah Heri na Khamis Mcha.
Wachezaji kutoka nje ya nchi aliyefika ni Mrundi Didier Kavumbagu pekee.
DOMAYO, BOKO WATUA SAUZI
Wachezaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, Frank
Domayo na Joseph Kimwaga wapo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa
vipimo vya majeraha yao.
Bocco ambaye ni mshambuliaji, anasumbulia na
maumivu ya goti, Domayo ambaye ni kiungo ana matatizo ya msuli wa paja
wakati Kimwaga anaumwa goti, naye ni mshambuliaji.
Daktari wa Azam FC, Mbaraka Twalib amesema:
“Wachezaji hao, wamekwenda kwa ajili ya vipimo vya juu ili kufahamu
maendeleo yao baada ya kufanyiwa matibabu.”
Mshambuliaji Kelvin Friday aliyekuwa mgonjwa pia naye ameanza mazoezi.
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
0 comments:
Post a Comment