KESHO Jumatano Yanga itawashusha nchini wachezaji wanne raia wa Zambia ambao mmoja wao ni kiraka wa TP Mazembe, Jonas Sakuwaha.
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imezipata jana
Jumatatu ni kwamba wachezaji hao watatu wanacheza ligi ya ndani huko
kwao, lakini mwenye nafasi kubwa na ambaye Yanga ina malengo naye ni
Jonas.
Habari zinasema kwamba mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 31, anaondoka Mazembe kwenda kutafuta changamoto mpya sehemu
nyingine kwa vile amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza
wanachocheza Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mmoja wa vigogo wa usajili wa Yanga aliidokeza
Mwanaspoti kwamba endapo mchezaji huyo atafuzu majaribio na kukubalika
na Marcio Maximo huenda Hamis Kiiza akaonyeshwa mlango wa kutokea kurudi
kwao Uganda.
Kiiza amekuwa hana wakati mzuri mbele ya Maximo
ingawa dakika chache anazochezeshwa huonyesha makali ya aina yake. Baada
ya kumtema Genilson Santos ‘Jaja’, wachezaji wa kigeni waliosalia
Yanga ni Mbuyu Twite, Andrey Coutinho, Kiiza na Haruna Niyonzima. Timu hiyo pia imetangaza ujio wa Mbrazili Emerson De Oliveira Neves Rouqe kwa majaribio ambapo atatua nchini kesho saa saba mchana sambamba na Maximo.

Mbali na wachezaji hao wawili wa kigeni wanaokuja
kwa majaribio, Yanga tayari imeshafanya mazungumzo ya awali na straika
wa Uganda na AS Vital, Yunus Sentamu.
Kikanuni Yanga ambayo imeanza mazoezi jana jijini Dar es Salaam inapaswa kuwa na wachezaji watano wa kigeni hivyo benchi la ufundi litalazimika kufanya uamuzi mgumu.
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo.

0 comments:
Post a Comment