Na Chikoti Cico
Huku kinyang’anyiro cha kugombania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia kikizidi kushika kasi kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani na timu ya Bayern Munich Manuel Neuer akata tamaa kushinda tuzo hiyo huku akimpa nafasi kubwa zaidi Christiano Ronaldo kunyakua kwa mara ya pili mfululizo.
Pamoja na kwamba kipa huyo anapewa nafasi pia ya kushinda tuzo hiyo kubwa duniani lakini bado binafsi anaamini taswira ya Ronaldo kwenye vyombo vya habari na ufundi wake uwanjani vinampa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo ya Ballon d’Or.
Akiongea na vyombo vya habari wakati Ujerumani wakijiandaa kucheza na Hispania kwenye mechi ya kirafiki kipa huyo alisema
“mimi ni mwanamichezo na sio balozi wa biashara, ukiachana na kuwa kipa namba moja wa Adidas, mimi sio mtu wa kupozi nikiwa na chupi, sipendi zulia jekundu napenda la kijani, najiskia vizuri nikiwa uwanjani nikijaribu kuwa bora ninavyoweza”
Neuer ambaye aliibuka kipa bora kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazili mwaka huu anaamini makipa wana nafasi ndogo sana ya kunyakua Ballon d’Or hasa ikizingatiwa kwamba mara ya mwisho kipa kunyakuwa tuzo hiyo ilikuwa ni mwaka 1963.
Akiongelea hilo Neuer alisema “Baada ya mchezo kitu wanachokionyesha zaidi ni magoli,nafasi za kufunga na pasi za magoli, watazamaji hawana kawaida ya kukumbuka kwamba kipa alizuia mipira migumu kwa kuchukua hatari kubwa ama kwa kupanga mchezo wa timu kutokea nyuma”
0 comments:
Post a Comment