Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 November 2014
Friday, November 07, 2014

Diego Costa na Juan Mata waachwa kikosi cha Hispania


Na Oscar Oscar Jr

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Hispania, Vicente Del Bosque ametaja majina ya wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya kufuzu Michuano ya Euro ambapo mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kucheza na timu ya taifa ya Belarus kisha, watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Dunia, timu ya Taifa ya Ujerumani.

Katika kikosi hicho, kuna majina ya wachezaji sita walioachwa na wengine kuchukuwa nafasi zao. Kiungo Juan Mata kutoka klabu ya Manchester United na mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ni kati ya wachezaji walioachwa kwenye kikosi hicho huku Isco kutoka Real Madrid na Jose Callejon wa klabu ya Napoli wakiitwa kwenye chama hilo.

Kitendo cha kumuacha Diego Costa kwenye kikosi hicho, kitapokelewa kwa furaha na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye hivi karibuni aliingia kweye tafulani na kocha Vicente Del Bosque juu ya matumizi ya mchezaji huyo ambaye afya yake bado haijatengemaa.

Hispania wako kwenye nafasi ya pili kwenye undi C baada ya kushuka dimbani mara tatu na kujikusanyia alama sita huku  Slovakia, wakiwa vinara wa kundi hilo wakiwa na alama tisa baada ya kushinda mechi zao zote.


Hii ndiyo orodha kamili ya wachezaji 23

Casillas, De Gea, Casilla, Juanfran, Azpilicueta, Ramos, Pique, Albiol, Bartra, Alba, Bernat, Busquets, Camacho, Koke, Cazorla, Fabregas, Callejon, Nolito, Morata, Alcacer, Pedro, Raul Garcia, Isco.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!