Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 November 2014
Tuesday, November 04, 2014

Jonas Mkude kutua Yanga?



KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima ni kama amemkaribisha kiungo wa Simba, Jonas Mkude kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kukiri kuwa ni mchezaji wa kiwango cha juu na ambaye anaweza kuisaidia timu kwa kiasi kikubwa.

Vigogo wa Yanga wamemuweka Mkude kwenye orodha yao baada ya kubaini kwamba mkataba wake unaelekea ukingoni na viongozi wa Simba hawajakaa kumuongezea kutokana na hali ilivyo ndani ya timu kwa sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti Niyonzima alisema Mkude ni aina ya wachezaji wenye vipaji vya kipekee na ambao wanaweza kufanya makubwa kwenye kikosi hicho cha Jangwani pale watakapopewa nafasi.

“Mkude ni mchezaji mzuri na ataisaidia Yanga endapo watamsajili, nitafurahi pia kucheza naye,” alisema Niyonzima kwa ufupi mara baada ya kutua Dar es Salaam jana akitokea Kagera ambapo aliishuhudia timu yake ikilala bao 1-0 kwa Kagera Sugar.

Wakati huohuo beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema licha ya kwamba atakosekana kwenye mchezo wa Jumamosi klabu yake hiyo itakapocheza na Mgambo JKT, bado wachezaji wenzake wataweza kupambana na kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi.

“Tunataka kwenda kwenye mapumziko tukiwa kwenye nafasi ya pili, tunafahamu kuwa ushindi wa mechi ijayo ni muhimu ili kutupandisha hapo, sitakuwepo lakini wenzangu wataweza kupambana.

“Yanga kuna mabeki wazuri ambao wanaweza kuziba nafasi yangu, pia morali ya timu iko juu baada ya kupata matokeo mabaya,” alisema Cannavaro.

Source: Gazeti la Mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!