Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 April 2014
Wednesday, April 02, 2014

USIKU WA ULAYA OLDTRAFFORD WAMALIZIKA KWA SARE 1-1



Kulikuwa na mechi mbili za mkondo wa kwanza wa robo fainali ya ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Jumanne usiku, Manchester United ya Uingereza ikikabana koo na mabingwa watetezi waligi hiyo Bayern Munich ya Ujerumani.

Nayo Barcelona ya Uhispania ikikabiliana na Athletico Madrid vilevile ya Uhispania.
Licha ya kuwa Bayern Munich ilikuwa imepigiwa upatu kutamba dhidi ya Manchester United vijana wa pep Gardiola walikabiliwa na ukuta mrefu wa Manchester uwanjani Old Traford.


Na walipopata fursa nahodha wa Manchester Nemanja Vidic alifunga bao maridadi la kichwa baada ya kuunganisha vizuri kona kutoka kwa Wayne Rooney kunako dakika ya 58 ya kipindi cha pili.
Gonga gonga ya Wajerumani ilikosa kuzaa matunda lakini bao la Bastian Schweinsteiger kunako dakika ya 66 iliwatunuku mabingwa hao wao watetezi bao muhimu la ugenini kabla ya mkondo wa pili utakaochezwa huko Ujerumani .

Bila shaka mashabiki na watani wa kocha David Moyes watakubaliana naye kuwa United itajutia fursa aliopoteza Danny Welbeck alipokuwa ni yeye pekee dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer .

United vilevile itamshukuru kipa David de Gea aliyefanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi haswa kutoka kwa Arjen Robben.

Kutokana na sare hiyo sasa mkufunzi Pep Guardiola ana kibarua kigumu pale Man United itakapozuru uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo.

Mechi nyingine 2 zimeratibiwa kuchezwa baadaye Jumatano, Real Madrid ya Uhispania ikivaana na Borussia Dortmund kutoka Ujerumani nayo Paris st Germain ikiikaribisha wawakilishi wengine wa Uingereza Chelsea ya Uingereza Katika uwanja wa Parc des Princes.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!