Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 April 2014
Wednesday, April 02, 2014

BARCELONA VS ATLETICO NAKO HAKUNA MBABE


Vita vya mahasimu wa nyumbani Atletico Madrid na Barcelona viliishia sare ya nne msimu huu timu hizo mbili za Uhispania zilipotoka sare ya bao moja kwa moja katika mkondo wa kwanza wa ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa katika uwanja wa Camp nou.
 
Atletico inayoongoza katika dimba la nyumbani ya la Liga sasa imejipatia bao muhimu la ugenini licha ya kuwa ilifuzu kuingia katika robo fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1997.

Licha ya barcelona kupigiwa upatu kushinda taji hilo ni Atletico iliyofunga bao la kwanza kupitia kwa kiungo Diego aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi yake Diego Costa aliyelazimika kuondolewa uwanjani
baada ya kupata jeraha katika dakika ya 30.

Barca ilifurukuta na kufunga baada ya Andre Iniesta kupenyeza pasi safi katikati ya ulinzi mkali wa Atletico iliyopokelewa na Neymar aliyesawazisha zikiwa zimesalia dakika 20 mechi hiyo kukamilika.

Juhudi za Barcelona za kutafuta bao la Ushindi ziliambulia patupu ngome ya ulinzi ya Atletico ilipoimarishwa na mambo yakasalia kuwa sare .
Athletico inaongoza ligi ya nyumbani kwa alama moja zaidi ya Barca.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!