Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

RNHIO RANGERS KUISIMAMISHA YANGA.




Ligi kuu Tanzania bara inaelekea mahali pazuri kwa wanaotaka ubingwa na wale wanaotaka kuepuka panga la kushuka daraja.Katika timu zinazowania ubingwa,huwezi kuwatoa Yanga na kwa upande wa kushuka daraja,huwezi kuwaondoa Rhino Rangers ya Tabora.Rinho Rangers,iliamua kuweka kambi ya siku 11 jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga ambao utachezwa keshokutwa Jumamosi na wachezaji wake wanataka kuishangaza nchi.
 
Rhino inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ilijificha katika kambi ya jeshi ya kikosi cha Twalipo, ikafanya mazoezi ya nguvu chini ya kocha, Jumanne Challe, kujiweka fiti kwa mchezo wao utakaochezwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Beki wa kati wa timu hiyo, Laban Kambole, ambaye mara kadhaa amekuwa akivaa beji ya unahodha, ameliambia Mwanaspoti kwamba waliamua kuweka kambi Dar es Salaam ili kujiweka vizuri na mchezo huo na kila mchezaji anawaza ushindi tu.
Beki wa zamani wa Yanga anayechezea Rhino, Ladslaus Mbogo alisema mchezo wao na Yanga utakuwa wa aina yake kwani kila timu imejiandaa vya kutosha lakini nafasi zao katika ligi zinachagiza ugumu wa mchezo.
“Tazama Yanga wanataka ubingwa hivyo hawatakubali kupoteza mechi, lakini sisi tunapambana kuhakikisha hatushuki daraja. Ushindi ni muhimu kwa kila timu,” alisema Mbogo.
Baada ya mechi ya jana ya Yanga dhidi ya Azam mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1,Yanga wameendelea kusalia nafasi ya pili wakifikisha alama 40 huku Azam wakiendelea kubaki kileleni wakiwa tayari wamejikusanyia alama 44.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!