Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

AZAM VS YANGA ZASABABISHA KIFO CHA SHABIKI.


Mambo bado magumu kuelekea mbiao za ubingwa Tanzania bara kati ya Azam na Yanga baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 jana Jumatano katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo ilikumbwa na tukio la huzuni baada ya shabiki mmoja wa Jangwani kufariki dunia uwanjani hapo.
 Yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia kwa straika wake Mrundi, Didier Kavumbagu, aliyemalizia mpira uliowababatiza mabeki wa Azam FC wakati wanaokoa shuti la fowadi mwenye nguvu Hamis Kiiza.
Yanga ambayo ni mabingwa watetezi, kwa matokeo hayo imefikisha pointi 40 na kusalia nafasi ya pili huku Azam ikifikisha 44 na kuzidi kujikita kileleni ikionekana kusisitiza kwamba haitulii mpaka itwae ubingwa wake wa kwanza la ligi hiyo.
Lakini Yanga baada ya kusikia tambo hizo, imeapa kwamba itapambana mpaka kieleweke katika mechi zake za nyumbani na ugenini zilizosalia kuhakikisha inalinda heshima yake na kupata tiketi ya kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Awali kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, alikuwa amewaambia wachezaji wake kwamba wasikubali kwa vyovyote kuiachia Azam pointi tatu akisema litakuwa kosa kubwa kwao. Lakini mpinzaniwake, Joseph Omog wa Azam alipoingia vyumbani wakati wa mapumziko huku Yanga ikiwa mbele, aliwaambia wachezaji wake kwamba wakomae na wasiipe Yanga nafasi ya kutawala mchezo.
Azam ambayo ni klabu pekee Afrika Mashariki inayomiliki uwanja wake binafsi unaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), ilisawazisha dakika ya 83 kwa shuti la Kelvin Friday aliyeunganisha pasi safi ya Aboubakary Salum ‘Sure Boy’. Friday aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Khamis Mcha.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!