Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

MOYES:MATA ATAZIBA PENGO LA ROBIN VAN PERSIE LEO
Meneja wa Manchester United David Moyes anaamini kwamba Juan Mata aliyenunuliwa pesa nyingi anaweza kuziba pengo la Robin van Persie wakati wa debi dhidi ya Manchester City uwanjani Old Trafford Jumanne. 

Van Persie ambaye ni straika wa Uholanzi anatarajiwa kuwa nje ya uchezaji wiki sita hadi nane kutokana na jeraha la goti ambalo huenda likaacha kiungo wa kati wa Uhispania Mata, ambaye alijiunga nao kutoka Chelsea kwa £37.1 milioni Januari, akicheza kati.

Tangu kutua kwa Mata, amekuwa akichezezwa winga ya kulia kuwezesha Moyes kutumia Van Persie na Wayne Rooney.
Moyes amefurahishwa na uchezaji wa Mata, hasa wakati wa ushindi wa 2-0 wakiwa West Ham Jumamosi na anatarajia afae zaidi wiki chache zijazo huku mabingwa hao wa Ligi ya Premia ambao wamehangaika msimu huu, wakiwa alama 11 kutoka nambari nne kwa sasa, wakijaribu kukwamisha juhudi za City za kushinda taji msimu huu. 

City kwa sasa wako namabri tatu.
"Hakuna klabu yoyote Ulaya au duniani ambayo haingependa kuwa na Robin van Persie akicheza kama fowadi wa kati na kwetu hilo ni pigo kubwa,” Moyes alikiambia kikao cha wanahabari Jumatatu.

"Alibadilisha mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (kwa kufunga mabao matatu wakati wa ushindi woa wa 3-0 mechi ya marudiano Old Trafford kabla ya kujeruhiwa huku United wakipata ushindi wa jumla wa 3-2 kwenye 16 bora dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki) kwa mabao aliyofunga lakini lazima niseme kwamba Juan Mata alikuja hapa kucheza nafasi mbili au tatu tofauti. 

“Ninafikiri Juan aliingia na kucheza vyema Jumamosi, Amecheza vyema katika mechi zote lakini Jumamosi alikaribia sana kufunga na labda angefunga mara kadha,” akaongeza Moyes kuhusu ushindi ambao Rooney aliwafungia mabao mawili. 

United walilazimika kutumia Michael Carrick beki ya kati wikendi kutokana na kutokuwepo kwa Jonny Evans, Chris Smalling, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand. 

Moyes hakueleza ikiwa mmoja wao atakuwepo mechi hiyo dhidi ya City ingawa Ferdinand anaweza kurejea baada ya kuuguza maumivu ya mgongo. 

Mdosi huyo kutoka Scotland, ambaye yuko msimu wake wa kwanza United baada ya kurithi mwenzake Alex Ferguson, meneja aliyefanikiwa zaidi kwenye soka la Uingereza, alisema hana wasiwasi kuhusu kumtumia Carrick katika nafasi hiyo tena na kwamba pia atatafakari uwezekano wa kutumia beki wa kushoto Patrice Evra, ambaye alipumzishwa wikendi, sehemu ya kati. 

"(Carrick) alifanya vyema kati na sina shida. Alikuwa amewahi kucheza hapo awali hivyo halikuwa tatizo. Hata tulikuwa tumetafakari kuweka (Marouane) Fellaini hapo tena, kwa hivyo tuna watu wa kutosha tukihitaji kufanya hivyo. 

“Tulimpumzisha Pat Evra na tukitaka, tunaweza kumuweka hapo na anaweza kufanya vyema. Ilikuwa vyema kwamba kikosi kiliweza.”
Ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal uwanjani Old Trafford Novemba ndio wakati pekee ambapo United wameilaza timu ambayo ni moja ya tisa zinazoongoza kwenye Ligi ya Premia msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!