Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

MOURINHO AMKATAA BALOTELLI

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho, amesema anaamini straika Mario Balotelli ataendelea kubaki kuwa mchezaji wa AC Milan na kwamba hafikirii hata chembe mpango wa kumsajili Mtaliano huyo kwa sababu si mchezaji anayemhitaji.

Staa huyo mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja, kwa siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua Stamford Bridge mahali ambapo Mourinho ni kocha mkuu.
Mourinho alisema anaamini Balotelli ataendelea kuichezea AC Milan, licha ya kwamba klabu hiyo kwa sasa mambo hayaiendei vizuri kwenye Ligi Kuu Italia.
Mourinho ambaye aliwahi kumnoa Balotelli walipokuwa pamoja katika klabu ya Inter Milan, alisema: “Mario anacheza kwenye moja ya klabu maarufu duniani.
“Clarence Seedorf (kocha wa AC Milan), naye anamhitaji sana, anahitaji muda pia na kutulia na wachezaji kama Balotelli. Naamini maisha ya Mario yataendelea kubaki Milan.”
Balotelli amefunga mabao 27 kwenye mechi 44 alizocheza tangu alipohama Manchester City mwanzoni mwa mwaka 2013.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!