Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

MOURINHO ASHITAKIWA NA FA

Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho ameshtakiwa na FA kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi ambapo timu hiyo yake ilishindwa 1-0 katika Ligi ya Premia na Aston Villa Jumamosi. 


Mourinho alifukuzwa uwanjani na refa Chris Foy kwa kuingia eneo la kuchezea baada ya kiungo wa kati wa Chelsea Mbrazil Ramires kuonyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja kwa kumchezea vibaya mchezaji wa kimataifa wa Morocco anayechezea Aston Villa Karim El Ahmadi.
"Jose Mourinho ameshtakiwa na FA kufuatia mechi ya timu yake dhidi ya Aston Villa Jumamosi 15 Machi 2014,” FA ilisema kupitia taarifa Jumatano. 

“Inadaiwa kwua kitendo cha meneja huyo wa Chelsea cha kuingia tena uwanjani mwendo wa dakika ya 90 wakati wa mechi hiyo na kumwendea refa ni utovu wa nidhamu.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!