Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 March 2014
Thursday, March 20, 2014

DROO YA ROBO FAINALI MABINGWA ULAYADroo ya robo fainali ya kombe la mabingwa Uropa itafanyika baadaye leo .
Timu nane ,Manchester United na Chelsea kutoka Uingereza ziatakuwa zikitarajia upinzani mkali ikikumbukwa kuwa.

mabingwa watetezi Bayern Munich walikutana na timu mwenza ya Ujerumani,Borussia Dortmund katika fainali za mwaka
uliopita. Lakini dakika tisini ndiyo itakayoamua mbivu na mbichi kwani kutakuwa na upinzani mkali kutoka vinara wa ligi kuu ya
Uhispania Real Madrid,Barcelona bila kuisahau Athletico Madrid zote hizo zinazoshikilia nafasi tatu za kwanza katika ligi
yao ya nyumbani la Liga.

Timu nyengine itakayosubiri kujua itachuana na nani ni Paris Saint Germain kutoka Ufaransa.
Mbali na timu hizo kushikilia nafasi nane bora miongoni mwa vilabu bara Uropa wadadisi wengi wa maswala ya kandanda
wanaipigia upatu Bayern Munich kuhifadhi taji lao .

Licha ya kushindwa katika fainali msimu uliopita Borussia Dortmund na Manchester United ndizo zinaosemekana kuwa
timu dhaifu kutokana na hali ilivyo katika ligi zao za nyubmani.

United imekuwa msururu wa matokeo duni katika ligi ya Uingereza na inashikilia nafasi ya Saba.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!