Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 March 2014
Sunday, March 23, 2014

KIUNGO WA DORTMUND KUSTAAFU SOKA.

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Sebastian Kehl atastaafu 2015 baada ya kutia saini nyongeza ya mkataba wake Jumapili hatua ambayo itamuweka Borussia Dortmund hadi mwisho wa msimu ujao, alisema Jumapili. 


Kiungo huyo wa kati wa miaka 34 alisema ana furaha kucheza msimu mwingine na kisha kutamatisha uchezaji wake katika klabu aliyojiunga nayo 2001.
"Borussia Dortmund, timu yetu kuu, mashabiki na jiji hili wamekuwa ni kama nyumbani kwangu kwa miaka mingi," Kehl alisema kupitia taarifa kutoka klabu hiyo. 

“Ndio maana nimeamua kuendeleza uhusiano huu lakini uamuzi nimeshafanya kwamba nitamaliza uchezaji wangu 2015. Natumai kwamba nitajivunia nyakati za kukumbukwa kwenye klabu hii na ufanisi mkubwa.” 

Kehl, ambaye amewahi kuchezea Hanover 96 na Freiburg, ameshinda mataji matatu ya ligi akiwa na Dortmund – ikiwa ni pamoja na ushindi wa ligi ya nyumbani 2012 na Vikombe Viwili. Dortmund pia walishindwa kwenye fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Bayern Munich msimu uliopita. 

Kehl alichezea Ujerumani mechi 31 c, na alicheza kwenye Kombe la Dunia 2002 na 2006 ambapo alifunga mabao matatu. Dortmund, ambao watachuana na Real Madrid katika robofainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, wamo nambari mbili Bundesliga na watakutana na Schalke 04 iliyo nambari tatu kwenye debi ya Bonde la Ruhr Jumanne.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!