Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 March 2014
Tuesday, March 25, 2014

ROBERTO MARTINEZ ATOFAUTIANA NA MOURINHO
Refa Andre Marriner ameponyoka kutimuliwa kutoka kwenye orodha ya Ligi ya Premia kwa kosa lake la kufukuza mchezaji kimakosa Stamford Bridge.
Refa huyo atasimamia mechi kati ya Southampton na Newcastle uwanjani St Mary's Jumamosi, kwa mujibu wa tangazo Jumatatu. 

Wakati viongozi wa Ligi ya Premia Chelsea wakiwararua wapinzani wao wa London Arsenal 6-0 Jumamosi, Marriner alimfukuza uwanjani Kieran Gibbs wa Gunners kwa kuunawa mpira badala ya Alex Oxlade-Chamberlain aliyekuwa ametenda kosa hilo. 

Eden Hazard aliiweka Chelsea 3-0 mbele kupitia penalti iliyofuata.
Marriner aliomba radhi kutokana na kosa hilo, ambalo lilipelekea meneja wa Blues Jose Mourinho kusisitiza ombi lake kwa marefa kuruhusiwa kutumia teknolojia ya video.
Hata hivyo, hilo halikumfurahishwa Clive Thomas, mmoja wa marefa walioheshimika zaidi kwenye soka la Uingereza. 

Huenda ni zaidi ya miaka 30 tangu raia huyo wa Wales wa miaka 77 aliyekuwa amebandikwa jina 'The Book' kwa kufuata kwa ukali kanuni za soka aliposimamia mechi kuu, lakini Thomas alisema Marriner na marefa wake wa mstari wanafaa kupigwa marufuku muda mrefu. 

"Ulikuwa uamuzi mbaya zaidi, na wa kushangaza zaidi ambao nimewahi kushuhudia,” Thomas aliambia BBC kabla ya Marriner kuteuliwa kusimamia mechi hiyo ya St Mary's.
"Kwa maoni yangu, wanne hao hawafai kusimamia mechi nyingine yoyote ya Ligi ya Premia msimu huu,” akaongeza Thomas. 

Hata hivyo, Dermot Gallagher – refa aliyestaafu majuzi – alitofautiana na Thomas na kusema Marriner, 43, hahitaji kufungiwa kwa muda mrefu.
“Sioni vile hilo linaweza kumfaa Andre,” Gallagher aliambia BBC.
"Huyo sio tu mmoja wa marefa wanaoongoza Uingereza bali pia Ulaya, na unataka kumpiga marufuku? Hilo halitasaidia Ligi ya Premia kwa sababu ni refa wa ligi ya juu – amefanya kosa moja na kujiamini kwake kutaathiriwa sana ikiwa hilo litafanyika,” akaongeza Gallagher, ambaye pia aliongea kabla ya kuthibitishwa kwa uteuzi wa Marriner kusimamia mechi. 

Kwenye taarifa iliyotolewa baada ya mechi hiyo, maafisa wa chama cha marefa walisema: “Andre ni refa mwenye ujuzi na bila shaka amesikitika sana kwamba kosa la kuchanganyikiwa kuhusu wachezaji lilitokea … Alieleza masikitiko yake kwa Arsenal alipofahamishwa kuhusu hilo.” 

Marriner alisimamia fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley mwaka uliopita ambapo Wigan walilazaManchester City 1-0.
Roberto Martinez, mdosi wa Wigan wakati huo ambaye sasa ni meneja wa Everton alimtetea refa huyo wa West Midlands lakini akapinga ombi la Mourinho kwamba marefa wawe wakisaidiwa na teknolojia.
"Ninafikiri teknolojia ya mstari wa goli ilikuwa hatua kuu, lakini kutoka hapo nadhani tunapaswa kuruhusu marefa wafanye kazi yao,” Martinez alisema. 

"Andre Marriner ana ujuzi mwingi na tajriba na hilo ni moja tu ya matukio ambao hutokea katika soka.
“Makosa ni sehemu ya mchezo huu na daima kutakuwa na makosa na maamuzi yasiyofaa lakini hiyo ni sehemu ya soka na lazima tukubali hilo kwani hilo ndilo hufanya soka iwe ilivyo,” Mhispania huyo akaongeza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!