Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 December 2013
Thursday, December 19, 2013

NIONAVYO MIMI:SITO SHANGAA KUONA KOCHA MAXIMO AKIRUDI KUIFUNDISHA STARS!


Na Oscar Oscar Jr


Rais Kikwete alikuwa na mtazamo wa mbali kabisa kumleta kocha Maximo.Wabogo tukamtusi,tukamkebehi na kila Mtanzania akawa anaweza kumchambua!

Wakati Maximo anajenga msingi,sisi wabongo tulikuwa tunataka apauwe! Mwisho wa siku akaondoka.Tust me,akirudi kuiongoza STARS kesho,wengi watamshangilia!!

Tatizo letu sio wavumilivu,tunapenda mafanikio ya haraka kwa njia ambazo si sahihi.Mechi moja tu ya "Nani mtani jembe" inaweza mpeleka Juma Kasseja benchi kama Barthez na Ivo kwenda kikosi cha Matola!

Kila kipa anapofungwa,inaaminika amehongwa na kila timu inapofeli kupata matokeo mazuri,basi kunawachezaji wamehujumu! Hili ni tatizo kubwa mno.

Badala ya kumleta Maximo kwa mara ya pili,ni bora tumwambie Kim Poulsen kwamba tunataka timu yetu ya Taifa itoke Uhai Cup,Umitashumta,umiseta,airtel Rising Star n.k na tunampa miaka 5 then tuone mafanikio.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!