Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2013
Friday, December 20, 2013

NIONAVYO MIMI:JOSE MOURINHO HAWEZI TIMIZA NDOTO ZA BOSI WAKE.

Na Oscar Oscar Jr

 
Roman Abromovic anataka vitu viwili kwa wakati mmoja na kwa Mourinho,anaweza kumpatia kitu kimoja tu.Wakati ameichukuwa chelsea kwa mara ya kwanza alimwita Mourinho kwa kazi moja tu,kuchukuwa taji la EPL na Mourinho alitimiza hilo.

Baada ya kupata ubingwa wa EPL,akawa anataka zaidi ubingwa wa ulaya.Di Mateo na Benitez wakaja na kumpatia.Nikadhani katosheka,mara nikasikia anataka timu icheze kama Barcelona!!

Chelsea ya Benitez ingeweza kutimiza ndoto za Roman Abromovic.Oscar,Mata na Hazard walikuta wametengeneza burudani ya hatari,huku Mikel na Ramires wakilinda vema beki ya kati kwenye midfield.

kaja huyu "bomoa bomoa" sioni dalili za kutimiza jambo hilo.Chelsea wakijaribu kupiga pasi nyingi,yeye ananuna! Anawaza magoli tu.Nadhani Bosi amuache tu jamaa atafute goli lake moja then alaze Bus lake chini otherwise,atakosa kila kitu.

Mourinho anaweza mataji tu,sio burudani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!