Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 December 2013
Thursday, December 19, 2013

NIONAVYO MIMI:HII NDIYO FANI NA MAUDHUI YA SIMBA NA YANGA.


Na Oscar Oscar Jr


Timu hizi kwa nje zinaonekana ni kama mali ya jamii lakini kiundani,hii ni biashara ya watu wajanja wanaotumia mashabiki lukuki wanaozipenda Club hizi kupiga pesa!

Siku wakipatikana watu wenye kuona fursa kwenye soka na wakawa tayari kuwekeza,simba na yanga watakuja kubaki na wakazi wa kariakoo tu.Pengine mashabiki wanabaki simba na yang
a kwa sababu hakuna mbadala!

Mh Lowassa kila siku anasema "vijana ni bomu linalo subiri kulipuka" nadhani kabla ya kulipuka hebu afanye investment kwenye soka la kisasa,ataokoa vijana wengi sana sio lazima wote tuitikie "kilimo kwanza"


Aden Rage ni kijisehemu tu cha tatizo la simba,ataondoka na tatizo litabaki pale pale.Yanga hawaongozwi na Aden Rage,wanamafanikio gani? Au kumleta Okwi na kurudi kwa Ngassa?

Sehemu kubwa ya soka la Tanzania ni kubadilishana,nani ale leo na nani aje kula kesho! Ataondoka Rage part one,atakuja Rage part two!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!