Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2013
Friday, November 15, 2013

PANDE MBILI ZA MTAZAMO WA SOKA.

NIONAVYO MIMI HIZI KAULI ZA WACHEZAJI,ZINA PANDE MBILI.


Na Oscar Oscar Jr.

Mshambuliaji wa Barcelona Alex Sanchez amesema,England haiwezi kuchukuwa kombe la Dunia 2014 Brazil kwa sababu wachezaji wake ni laini(soft).

Namwangalia Micar Richards,Namuangali Jack Wilshere,namuangalia Ashley Cole na upande wa pili namuangalia Wyne Rooney,nagundua kabisa kwamba,hawa sio "soft" Nampinga Alex Sunchez!

baadae,naangalia madudu ya Joe Hart,naangalia utu uzima wa Lampard na Gerrard kisha sioni mbadala wa hao watu.Nikifika kwenye hii point,nakubaliana na Sanchez!

Steven Gerrard kasema,Luis Suarez ni mshambuliaji hatari zaidi kuliko Torres ukichezanae.Anadhani ubora wa Torres yule wa liverpool huwezi linganisha na Suarez.

Nikimkumbuka El-nino yule mwekundu namna alivyokuwa analijua goli,nampinga Gerrard.

Baadae nakumbuka kwamba,Torres alicheza zama za Alonso Original na Gerrard Original na kwa sasa,Suarez anacheza kwa Gerrad fake na Henderson Fake.Nikifikia hii point,nakubaliana na Gerrard.

I'm sorry!


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!