Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2013
Friday, November 15, 2013

TFF NA KITENDO CHA KUFUNGIA WIWANJA VIBOVU TANZANIA

NIONAVYO MIMI KUFUATIWA KUFUNGIWA KWA BAADHI YA VIWANJA NCHINI.


Na Oscar Oscar Jr.
Huwa inatokea mzozo sana kwa sisi tunaokaa nyumba za kupanga,unataka kupakiwa rangi chumba chako,mwenye nyumba hana time! Unataka kufungiwa feni,mwenye nyumba hana time! Mwisho unaamua ama ubaki hivyo hivyo au ukatafute nyumba nyingine ukapange!!

Kamati ya Bodi ya Ligi imevifungia baadhi ya viwanja kutokana na kutokuwa na ubora lakini viwanja hivi ni mali ya Chama Tawala na chama tawala hakina mpango wa kuviboresha,na timu zinazokodi viwanja hivi,hazina mpango wa kujenga vya kwao.Hapa patamu sana!!

Simba na Yanga wanaweza wakawa wanacheka tu kwa sababu jambo hili haliwaathiri,ila tukibadili mawazo tunaweza tukagomea uwanja wa Taifa nao upumzishwe ili sisi wa mikoani na nyie wa kiriakoo,wote tukawapigie magoti Azam pale Chamazi!!

Hivi nani anatakiwa kuviboresha ni TFF,Chama Tawala au timu zinazolipia kodi kila wanapovitumia??

Natamani kusikia mwenyekiti wa hicho chama akisema kuwa hawatoviboresha kwa sababu chama kinataka kuanzisha mradi wa kuku,hivyo basi wapenda mpira wajenge vya kwao!!

I'm sorry!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!