Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 September 2013
Thursday, September 19, 2013

HAYA NI MAISHA YA KIZAMANI KATIKA SOKA.



                                             azam fc


Watanzania timu zetu za mikoani mtaji wao ni sisi wa mikoani.Hata ije kutokea mkoa wa shinyanga ukaipandisha timu ya MWADUI na ikafikia mafanikio kama ya MANCHETSER UNITED,hakuna mtu anayetoka dar atakuja kuishangilia hiyo timu.

Wakati YANGA ikifanyiwa vurugu jijini mbeya,nilishangaa kuona watu toka KIGOMA nao wanasema MBEYA CITY COUNCIL watakoma wakija dar kucheza na YANGA!! Nikawa najiuliza,hivi kwanini hawa watu wasiishangilie na kuichangia timu yao toka kibondo ya JKT KANEMBWA ili msimu ujao icheze VPL?

Juzi nimemsikia kocha mmoja toka kanda ya ziwa ambaye timu yake inashiriki ligi daraja la kwanza akilalamika kwamba kuna wachezaji wake wawili toka NIGERIA hawakupata ITC na hivyo ni pigo kwa timu yake.Hivi mpaka daraja la kwanza tunahitaji watu kutoka nje??
                                                                                              
kwa nini tunawanyima fursa watanzania ambao pengine wanavipaji kuliko hata hao kina OBI OKONKWO? Nilichogundua ni kwamba,hatuendi wilayani na kwenye tarafa zetu kuwatafuta watoto wetu wenyewe.

kwa zama hizi binafsi,nilikubali ujio wa OKWI jembe hili toka UGANDA kutua msimbazi na fundi wakinyarwanda NIYONZIMA pande za jangwani,hawa wengine nina amini tunao mikoani sema tu hatutaki kuwatafuta.


                                           mtibwa sugar
i'm sorry.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!