Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 May 2013
Monday, May 27, 2013

MANCHESTER UNITED VS BAYERN MUNICH FAINAL 1999

                                                                

Mwaka 1999 kuna fainal kubwa ya EUFA CHAMPIONS LEAGUE ilipigwa kule spain katika dimba la NOU CAMP kati ya man united vs Bayern munich.United kama kawaida walimkosa captain wao ROY KEAN na kiungo wao hodari PAULO SCHOLES kutokana na vizuizi walivyokuwa navyo.
Mechi ilichezeshwa na mtaliano  PIERLUGINA COLLINA na man of the match aliibuka MARIO BASLER wa BAVARIANS.

The BAVARIANS waliingia katika fainal hiyo huku wakimkosa mshambuliaji wao hatari toka BRAZIL Elber Giovani na beki wao wa kutumainiwa mfaransa BIXENTE LIZARAZU.
Dk ya 6 tu ilishuhudia beki wa united Johnsen  akimchezea madhambi mshambuliaji wa BAVARIANS Jancker.COLLINA aliamuru ipigwe mpira wa adhabu na Mario Basler aliweza kukwamisha mpira huo wavuni.

goli lilidumu hadi dakika ya mwisho ya 90,huku united chini ya sir Alex Ferguson ikifanya mabadiliko ya kuwaingiza ndani TEDDY SHERINGHAM na OLE GUNNAR SOLSKJEAR.mwamuzi msaidizi akaonyesha dakika 3 za nyongeza na hapo ndipo BAVARIANS walipoumia.dakika ya 90:36 Teddy sheringham alisawazisha na Bayern wakiwa wamechanganyikiwa dk ya 92:17 Ole Gunnar Solskjear akawapa united goli la 2 na mpira ukamalizika huku watoto wa The Bavarians wakiwa wamelala chini bila kuelewa kilichotokea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!