by Joachim Sologo
.
Kwa
wale waliobakia katika runinga zao au kumbi za mpira watakubaliana na mimi
kwamba Arjen Robben alionekana kuwa mwenye furaha nathubutu kusema kuliko wachezaji
wote wa Bayern Munich. Akiwa amezaliwa tarehe 23 January mwaka 1984 katika nchi
ya Uholanzi, Arjen Robben ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu anayemudu
vyema nafasi ya winga (kiungo mshambuliaji). Arjen Robben amepitia katika timu
tofauti tofauti, alianza kucheza soka lake katika timu ya nyumbani kwao iitwayo
Groningen katika msimu wa 1999/2000.
Baada
ya kupata umaarufu akiwa na timu hiyo ARjen Robben alinunuliwa na club ya PSV
ambayo aliitumikia kabla ya matajiri wa uingereza wenye maskani yao pale
darajani Chelsea almaarufu The Blues kumchukua wakati huo wakiwa chini ya
kibopa wao Bilionea Abramovich na mwalimu wao msema ovyo Jose Mourinho. Baada ya kuitumikia
Chelsea kwa mafanikio hatimaye Arjen Robben alihamia Real Madrid ambako hakuwa
na msimu mzuri sana kutokana na kuandamwa na majeruhi, lakini kwa sababu
anayejua anajua tu siku zote fundi huyu Arjen Robben hatimaye alitua katika
mikono salama ya wanaume kutoka Ujerumani ambao ni Bayern Munich klabu
anayoitumikia hadi sasa.
Kwa nini Robben
alifurahi sana jana?
Kwangu mimi nimefanya tathmini ya mambo machache ambayo nahisi yalimfanya
Robben kufurahia sana ubingwa wa UEFA hapo siku ya jana. Anagalia yafuatayo;
Kabla
ya fainali ya jana Arjen Robben alikuwa amepoteza fainali nne za makombe
makubwa ndani ya miaka mi 4 hivyo alijiona kama mtu asiye na bahati. Kumbuka
kabla ya fainali ya jana Robben alikuwa amepoteza fainali kubwa nne ambazo ni
ile ya Kombe la dunia nchini Afrika Kusini dhidi ya Hispania mwaka 2010,
fainali mbili za UEFA champions league ambazo ni ile dhidi ya Inter Milan mwaka 2010 na ile ya mwaka jana 2012 dhi ya
Chelsea lakini pia usisahau kwamba akiwa na Bayern alikosa kombe la DFB Pokal katika
fainali.
Robben
alikosa mkwaju wa penalt katika fainali ya mwaka jana pale jijini Munich katika
uwanja wa Allianz Arena, ilikuwa ni penalt ambayo kama angeifunga katika
fainali ile basi Bayern Munich wangeweza kutawazwa mabingwa mwaka jana mbele ya
Chelsea. Hiyo ilimfanya kukosa raha na kujiona mnyonge mbele ya mashabiji wa
timu yake hiyo.
Katika
mchezo wa jana tayari alikuwa ameshakosa nafasi tatu muhimu, hivyo ni wazi
kwamba kama Bayern Munich wasingetwaa ubingwa hapo jana basi Arjen Robben
angepaswa kubebeshwa lawama maana alipata nafasi muhimu lakini hakuwa makini
katika kuzitumia.
Kutwaa
ubingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza, kombe la jana ndilo lilokuwa la kwanza kwa
Arjen Robben katika ngazi ya vilabu barani ulaya. Hivyo ilikuwa usiku wa pekee
katika maisha yake ya soka.
Huyu
ndiye Arjen Robben, shujaa wa Bayen Munich katika fainali ya UEFA champions
League iliyopigwa jana pale katika uwanja wa Wembley katika jiji la London
ambako shujaa huyu alipata kuishi wakati akiitumikia Chelsea watoto wa
darajani. Haya yote yalimfanya kuwa mtu mwenye furaha baada ya filimbi ya
mwisho iliyoashiria kuwa BAYERN MUNICH ndiyo mabingwa wapya wa UEFA CHAMPIONS
LEAGUE 2012/2013.
0 comments:
Post a Comment