Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2017
Wednesday, February 01, 2017

MOURINHO AMUONYA MARTIAL




Na FLORENCE GR

Kocha wa klabu ya Manchester united  Jose Mourinho amemuonya Anthony Martial na kumtaka kupandisha kiwango kwani mchezaji anaecheza nae namba moja Henrikh Mkhitaryan yupo nyuma yake anamuangalia tu.

Martial amabe amekuwa katika wakati mgumu tangu alipowasili Jose Mourinho msimu huu huku akifanikiwa kufunga magoli mawili tu mpaka sasa hali liliyopelekea kusambaa kwa taarifa  kuwa kunauwezekano wa mfaransa huyo kuondoka kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa jana usiku.

Akiongea na waandisahi wa habari kuelekea mechi yao dhidi ya Hull city Usiku wa leo Mourinho amesema kuwa ' sasa inatosha kukaaa benchi , anatakiwa aonyeshe kiwango zaidi ya anaeshindana nae'

Mourinho aliendelea kusema kuwa' nafasi yake tuna wachezaji wengi wa kucheza, Unataka nimuache nje  Mkhitaryan ambae alikuwa mchezaji bora wa mechi (dhidi ya Wigan kwenye kombe la FA)? siwezi kufanya hivyo.

' Wachezaji wanajichagua wenyewe me nipo kwa ajili ya kuchambua kile wanachofanya uwanjani na kujaribu kutokuwa na upendeleo kwa yoyote,kwa kiwango kile alichoonyesha Mkhitaryan dhidi ya Wigan atacheza tu dhidi ya Hull city '

Manchester united inatarajia kucheza na Hull city usiku wa leo kwenye mchezo wa ligi kuu Uingerza ikiwa katika nafasi ya sita na pointi 41 baada ya mechi 22 huku hull city ambayo walifanikiwa kuifunga Manchester united magoli 2-1 katikati ya wiki iliyopita kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la ligi wapo nafasi ya mwisho kabisa ya msimamo wakiwa na pointi 16 tu katika mechi 22.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!