UZOEFU UMETUBEBA- GRANT
Na FLORENCE GR
Mabingwa mara nne wa AFCON timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Gabon mara baada kuifunga timu ya taifa ya DR Congo mabao 2-1 katika robo fainali ya tatu iliyokuwa nzuri kuitazama kutokana na timu zote mbili zilivyokuwa zinacheza.
Wakicheza bila ya nahodha wao Asamoah Gyan ambaye bado ni majeruhi vijana wa Ghana wakiongozwa na wana wa familia moja Jordan Ayew na Andre Ayew ndo waliokuwa mashujaa wa timu yao mara baada ya kila mmoja kufunga goli moja na kuiwezesha timu hiyo kutinga nusu fainali ambapo watapambana dhidi ya Bukina Faso siku ya Alhamisi.
Akiongelea mchezo huo kocha wa Ghana Avram Grant alisema kuwa uzoefu ndo umeibeba timu yake kuibuka na ushindi huo huku akisititiza kuwa kipindi cha kwanza hawakuweza kucheza vizuri na walipoteza nafasi mbili ambazo timu ya DR congo walianzisha mashambulizi ya kushtukiza lakini wachezaji wake wazoefu walifanikiwa kuokoa hatari hizo.
Grant aliendelea kusisitiza kuwa kipindi cha kwanza DR Congo wlikuwa watulivu sana hivyo kuwapa wakati mgumu wachezaji wake hivyo kusahihisha makosa yao na kufanikiwa kufunga magoli kunako kipindi cha pindi.
DR Congo walitawala kipindi cha kwanza huku nyota wake Dieumerci Mbokani na Junior Kabananga wakikosa nafasi za wazi walizozipata .
Grant alimalizia kwa kusema kuwa ' walifunga goli zuri sana pale tulipokuwa tumelala na si rahisi kucheza dhidi ya DR Congo ,ni timu nzuri inacheza,wachezaji wake wanajua jinsi ya kujipanga na wamefunga magoli mengi mpaka sasa lakini tumecheza vizuri sana kipindi cha pili na kupata matokeo'
0 comments:
Post a Comment