Na George Mganga
Ulimwengu wa soka kwa miaka ya karibuni
umetawaliwa na wachezaji wawili, mmoja wa
FC Barcelona na mwingine ni mkali toka kikosi
cha Real Madrid .
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa
pamoja wamekuwa katika kiwango ambacho
kimewafanya waonekane kama watu
wanaotoka kwenye sayari nyingine hali
ambayo imezua upinzani kati yao.. story zao
huwa hazikauki na kwenye HEADLINES za
michezo, hata vijiweni pia.
Moja ya hoja ambazo zimekuwa zikiibuka ni
nani kati ya wawili hawa ni bora kuliko
mwingine, hoja hii imezaa swali jingine
miongoni mwa watu ya kwamba ingekuaje
kama wachezaji hawa wangekuwa kwenye
timu moja??
Ni vigumu kwa hili kutokea kwani kwa sasa
wanacheza kwenye timu zenye utamaduni wa
upinzani na wanakoelekea ni vigumu kuona
wakibadilishana timu siku moja yaani eti
kumuona Ronaldo akichezea Barcelona na
Messi akichezea Madrid ??
Sio hapo tu.. hata kwenye timu ya taifa
uwezekano huo haupo kwani Messi ni
Muargentina na Ronaldo anatoka Ureno.
Jarida la Mundo Deportivo limeripoti mpango wa
kuandaa mchezo maalum wa wachezaji nyota
barani ulaya .
Hata hivyo ndoto ya wawili hawa kuonekana
wakichezea timu moja huenda ikawa kweli
baada ya jarida moja la Hispania Mundo
Deportivo kuripoti mpango wa kuandaa
mchezo wa wachezaji nyota toka klabu
mbalimbali barani ulaya.
Hii imetokana na wazo kama la mchezo wa
Ligi ya Basketball Marekani NBA, yaani NBA
All Star ambapo wachezaji huchaguliwa na
kuwakilisha kambi za mashariki na magharibi
na kwa Ulaya zitachaguliwa timu mbili
zikiwakilisha wachezaji toka vilabu vya Ulaya
Kaskazini na Kusini.
Wazo hili litahusisha wachezaji
watakaochaguliwa na mashabiki kupitia
mtandao ambapo kutakuwa na wastani wa
wachezaji watatu toka klabu moja na hapa
ndio uwezekano wa kuwaona Messi na
Ronaldo wakiwakilisha Hispania ambayo iko
kwenye eneo la kusini mwa Ulaya.
Wachezaji wengine nyota kama Zlatan
Ibrahimovic , Gareth Bale, Neymar na Edinason
Cavanni pia wanaweza kujumuishwa kwenye
kikosi cha Ulaya Kusini ambacho kitakuwa na
klabu za mataifa kutoka Ureno, Hispania na
Ufaransa.
Wachezaji kama Wayne Rooney, Angel Dim
Maria, Sergio Aguerro , Alexis Sanchez na Edin
Hazard pamoja na wachezaji nyota wa Bayern
Munich watawakilisha kikosi cha klabu za
Ulaya Kaskazini.
Hata hivyo bado wazo hili halijawa rasmi na
haijafahamika kama litafanyiwa kazi kikamilifu
na kuweza kutimiza azma ya mashabiki ya
kuona mkusanyiko wa wachezaji nyota wakiwa
wanacheza kwenye timu moja.
Story ni kwa mujibu wa Millard Ayo
0 comments:
Post a Comment