Na George Mganga
Kocha wa kilabu ya Borrusia Dortmund Jurgen
Klopp amesema ataondoka katika kilabu hiyo
mwishoni mwa msimu huu.
Mkufunzi huyo wa miaka 47 kutoka Ujerumani
alitaka asimamishiwe kandarasi yake ambayo
ilitarajiwa kukamilika mwaka 2018.
''Sio kwamba nimechoka,sijakuwa na mawasiliano
na kilabu yoyote,lakini sina mpango wa kuchukua
likizo''.alisema.
Kocha Jurgen Klopp akiwa na wachezaji wake
wa kilabu ya Dortmund
Klopp ameifunza Dortmund tangu mwaka 2008,na
kuwasaidia kushinda mataji mawili ya ligi mbali
na kucheza katika fainali za kombe la kibalu
bingwa ulaya mwaka 2012-13,lakini sasa wako
katika nafasi 10.
Kwa sasa wako pointi 37 nyuma ya viongozi wa
ligi ya Ujerumani Bayern Munich.
Klopp ameuambia mkutano na waandishi wa
habari: '' nilikuwa nikisema kwamba ninaamini
mimi sio mkufunzi mzuri zaidi katika kilabu hii''.
0 comments:
Post a Comment