Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2015
Sunday, February 01, 2015

Henry aipa Chelsea ubingwa.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka kwenye studio za Sky Sports nchini Uingereza amedai Chelsea inaweza kunyakua ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwasababu Jose Mourinho anajua kuepuka kufungwa wakati timu yake ikicheza vibaya.
Henry alizungumza hayo wakati akichambua mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City uliopigwa jana, mchezo ulioisha kwa sare ya goli 1-1 huku goli la Chelsea likifungwa na Loic Remy kabla ya David Silva kuisawazishia Manchester City. Pamoja na sare hiyo lakini City walikuwa bora zaidi kuliko Chelsea na Henry anaamini Chelsea walionyesha ishara ya bingwa wa ligi ya Uingereza.
Henry akiongea baada ya mchezo huo alisema “Tuwape (Manchester City) pongezi. Nani walichukua alama kwenye uwanja wa Bridge mwaka huu? Hakuna”. Walikuja mchezoni, walimiliki mpira, nafasi zadi, hawakushinda lakini unacheza dhidi ya Chelsea. Walichukua alama, wangeweza kufanya zaidi? Labda”.
“Hivyo ndivyo Chelsea hufanya, wanaweza wasicheze vizuri wakati mwingine lakini wanshinda 1-0. Walihangaika leo, hawakupoteza na ndiyo maana ni timu ambayo nadhani watakuwa mabingwa. Naamini hilo, kwangu ni wajasiri sana, wanaweza kushinda wakati hawachezi vizuri hiyo ni ishara ya mabingwa kwa kawaida”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!