Swansea City yafundisha watu mpira
Na Florence George
Mabao mawili kutoka kwa Bafetimbi Gomis, yalisaidia timu yake ya Swansea City kuibuka na ushindi wa goli 6-2 dhidi ya wenyeji wao timu ya Tranmere Rovers inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza katika mchezo wa kombe la FA uliocheza siku ya jumamosi.
Wakiwa bila ya mchezaji wao muhimu Wilfried Bony, Swansea walitawala mpira kwa asilimia 80 dhidi ya timu hiyo huku Nathan Dyer alikuwa wa kwanza kuifungia Swansea goli la kwanza kabla ya Modou Barrow na Tom Carroll kufunga magoli mawili mapema mwa kipindi cha pili.
Tranmere walijitahidi na kufanikiwa kupata magoli mawili kupitia kwa Power na Stockton,huku magoli mengine ya Swansea yakiwekwa kimiani na Gomis aliyefunga mawili kabla ya
Routledge aliyeingia akitokea benchi kuhitimisha idadi hiyo ya magoli.
Kwa matokeo hayo sasa Swansea ambayo ipo katika nafasi ya 9 ikiwa na pointi 29 katika msimamo wa ligi kuu, imefanikiwa kutinga katika hatua ya nne ya kombe hilo.
0 comments:
Post a Comment