Saido Berahino Haendi kokote kule
Na Florence George
Mwenyekiti wa klabu ya soka ya West Bromwich Albion ya nchini Uingereza Jeremy Peace, amesema kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza ayeichezea timu hiyo Saido Berahino kuwa hawezi kuuzwa katika kipindi hichi cha uhamisho wa wachezaji japokuwa amekuwa akihusishwa kuhitajiwa na timu kubwa nchini humo.
Berahino amekuwa mchezaji muhimu katika timu hiyo ambapo hadi sasa ameshafunga magoli 14 katika michezo 26 aliyoichezea timu hiyo katika mashindano mbalimbali msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifanikiwa kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza mwezi November kutokana na kiwango alichoonyesha uwanjani na amekuwa akuhusishwa kuhitajiwa klabu za Liverpool na Tottenham Hotspur za nchini Uingereza.
Akiongelewa suala hilo Jeremy Peace aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo mwezi huu wa January na wanamuachia suala hilo kocha wa timu hiyo Tony Pulis.
Pia mwenyekiti huo alizungumzia kuondoka kwa wachezaji Sebastian Blanco na Silvestre Varela katika kipindi hiki cha usajili,alifafanua kuwa dili ya Varela kwenda kwa mkopo katika timu ya Fc Porto ya Ureno lilishindikana huku Blanco akitarajiwa kujiunga na timu ya San Lorenzo ya Nchini Argentina .
0 comments:
Post a Comment