Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa Everton Mkameruni Samwel Etoo anatarajia kujiunga na klabu ya Sampdoria inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A baada ya timu hiyo kufikia muafaka na wakala wa mchezaji huyo.
Etoo mwenye umri wa miaka 33 ambaye bado ana makazi jijini Milan amepewa mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu ya Sampdoria huku kukiwa na matarajio ya kuwa kocha wa timu hiyo baada ya mkataba wake kuisha.
Wakati huo huo viongozi wa klabu ya Sampdoria wanataka kukamilisha mapema dili la usajili wa Etoo mapema iwezekanavyo kati ya Jumatatu na Jumanne ili mshambulaji huyo aweze kucheza mchezo wa kombe la Italia siku ya Jumatano dhidi ya timu yake ya zamani Inter Milan.
0 comments:
Post a Comment