Na Chikoti Cico.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Mfaransa Thierry Henry ataangaza rasmi kuondoka timu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani ijulikanayo kama Major League Soccer.
Henry amefikia uamuzi huo baada ya kuichezea timu hiyo kwa muda wa miaka minne na nusu toka alipojiunga nayo mwaka 2010.
Henry ambaye ameshawahi kuzichezea timu za Monaco, Juventus, Arsenal na Barcelona anaondoka huku akiwa ameichezea timu ya Red Bulls mechi 122 na kuifungia jumla ya magoli 51.
Baada ya mechi ya Red Bulls dhidi ya New England Revolution siku ya Jumamosi ambayo Henry alicheza ndipo mchezaji huyo alipotangaza kuwa huo ulikuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na jezi za timu hiyo.
Akitangaza rasmi kuiacha timu ya Red Bulls Henry alisema “nachukua nafasi hii kutangaza kwamba bahati mbaya mchezo wa Jumamosi ulikuwa wa mwisho kwangu kwa New York Red Bulls.
Uamuzi mara zote ulikuwa hivyo kwamba ntaondoka baada ya kipindi cha mkataba wangu na ingawa hilo kamwe haliwezi kubadilika, sikutaka lisumbue kwenye maendeleo ya timu”
Henry aliendelea kwa kusema “ninyi mna maana kubwa sana kwangu na nawashukuru kwa kuniunga mkono vizuri, ntachukua wiki chache zijazo kuwaza na kuamua ukurasa unaofuata kwenye kazi yangu. Asanteni”.
Wakati huo huo baada ya kutangaza kuiacha timu ya Red Bulls Henry alibadilisha mwonekano wa ukurasa wake wa Facebook kwa kuweka picha ya uwanja wa Emirates jambo linalochochea taarifa za mchezaji kutaka kurejea Arsenal akiwa kama sehemu ya benchi la ufundi.
0 comments:
Post a Comment