Real Madrid vs Celta Vigo, pale Santiago Bernabeu
Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Real Madrid haijapoteza mchezo wowote nyumbani kwa kipindi cha miezi mitatu sasa na siku ya Jumapili, watakuwa kwenye dimba la Nyumbani Estadio Santiago Bernabeu kuumana na timu ya Celta Vigo ambayo msimu huu ilifanikiwa kuwazui Barcelona, Atletico Madrid na Athletico Belbao.
Barcelona ndiyo timu ambayo imewahi kucheza mechi nyingi (18) katika historia ya klabu za Hispania pasipokupoteza mechi. Real Madrid kwa sasa, wameshinda mechi 17 kwenye mashindano yote bila kupoteza na wakishinda mchezo wao dhidi ya Celta Vigo, watakuwa wanaifikia rekodi iliyowekwa na Barcelona.
Christiano Ronaldo, Karim Benzema, Gareth Bale, Ramos, Carvajal, Marcelo na Pepe wote walipumzishwa kwenye mchezo wa kombe la Mfalme na hivyo wanatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancelotti siku ya Jumapili dhidi ya Celta Vigo.
Celta vigo ambao wanakamata nafasi ya saba kwenye La Liga wakiwa na alama 20, wanarekodi nzuri wanapocheza Santiago Bernabeu kwani katika mechi saba za hivi karibuni, wamepoteza michezo mitatu pekee, wamepata sare mechi mbili na kushinda mara mbili.
Celta Vigo wamekuwa wanachechemea kwani katika mechi nne za hivi karibuni wamejikuta wanapoteza mechi tatu na kutoka sare mchezo mmoja huku, ushindi wao wa mwisho ni ule wa kuifunga Barcelona bao 1-0 Septemba mosi.
Real Madrid wanahitaji alama tatu kwenye mchezo huo wa 40 kwa kocha Carlo Ancelotti tangu alipochukuwa mikoba ya Jose Mourinho ili kuongeza wigo baina yao na Barcelona ambao wanawafukuzia kwa karibu mno.
Real wanapointi 33, Barcelona 31 huku Atletico Madrid wao wakisalia na alama 29.
0 comments:
Post a Comment