Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

Makocha watatu tu ndiyo wazawa AFCON 2015


Na Oscar Oscar Jr


Michuano ya mataifa ya Afrika ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi kule nchini Guinea ya Ikweta mapema mwezi Januari, itashirikisha mataifa 16 kutoka bara la Afrika. 

Katika mshangao wa wadau wengi, michuano hiyo itakuwa na makocha watatu tu ambao ni wazawa na raia wa bara la Afrika. Mara ya mwisho kwa michuano ya bara la Afrika kushuhudia makocha wengi wazawa, ilikuwa kwenye fainali zilizofanyika nchini Mali mwaka 2002.

Nchi za Afrika zimekuwa na utamaduni wa kuwakumbatia makocha wengi wa kigeni na kushindwa kutoa nafasi kwa wazama kitu ambacho kinatajwa kama moja ya sababu zinazopelekea soka la bara letu kushindwa kupiga hatau. 

Ni nchi za Zambia, Congo DRC na Afrika Kusini pekee ndiyo waliowapa imani makocha wazawa lakini mataifa yaliyobaki yote, yatakuwa na makocha wakigeni.

Mwaka 2008 wakati michuano hiyo ikipigwa nchini Ghana, Mataifa 11 kati ya 16 yaliongozwa na makocha wakigeni lakini awamu hii, ni rekodi ambayo haijawahi kutokea tangu michuano hiyo ilipoongezwa timu shiriki na kufikia 16.

Orodha ya makocha AFCON 2015

South Africa: Ephraim Mashaba (South African)
Algeria: Christian Gourcuff (French)

Burkina Faso: Paul Put (Belgian)

Cameroon: Volker Finke (German)

Cape Verde: Rui Aguas (Portuguese)

Congo: Claude Le Roy (French)

Ivory Coast: Hervé Renard (French)

Gabon: Jorge Costa (Portuguese)

Ghana: Avram Grant (Israeli)

Guinea: Michel Dussuyer (French)

Equatorial Guinea: Andoni Goikoetxea (Spaniard)

Mali: Henryk Kasperczak (Polish)

DR Congo: Florent Ibenge (Congolese)

Senegal: Alain Giresse (French)

Tunisia: Georges Leekens (Belgian)

Zambia: Honour Janza (Zambian)

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!