Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili na Chelsea, Oscar Dos Santos amesaini mkataba mpya na timu ya Chelsea ya kutoka jijini London, mkataba utakaombakisha kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2019.
Oscar aliyesajiliwa na Chelsea mwaka 2012 toka timu ya Internacional ya nchini Brazili amesaini mkataba mpya wa miaka mitano huu ukiwa ni msimu wake wa tatu toka aliposajiliwa huku akifunga jumla ya magoli11 kwa msimu uliopita.
Baada ya kusaini mkataba huo mpya Oscar akiongea na mtandao wa Chelsea alisema “Ninafuraha kwasababu napenda kuichezea Chelsea na kuishi Uingereza. Nimefurahia kucheza hapa kwa miaka miwili na sasa nina miaka mitano zaidi hivyo nina furaha sana”
Mpaka sasa Oscar amefunga magoli 27 katika mechi 92 alizoanza na katika mechi 34 alizoingia kama mchezaji wa akiba huku kwenye msimu huu mpya akicheza mara 15 katika mashindano mbalimbali ambayo Chelsea imecheza na kufunga magoli manne pia mpaka sasa ameichezea timu ya taifa ya Brazili michezo 40 na kufunga magoli 11.
Huku akivaa jezi namba nane iliyokuwa inavaliwa na kiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard Oscar ameisaidia timu hiyo kutoka London kuongoza ligi ikiwa na alama 32 mpaka sasa baada ya kushinda michezo 10 na kutoka sare michezo miwili huku ikiwa haijafungwa toka kuanza kwa msimu wa 2014/2015.
0 comments:
Post a Comment