Alexies Sanchez ni sawa na Luiz Suarez.
Na Oscar Oscar Jr
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameibuka na kumlinganisha mshambuliaji wake Alexies Sanchez na mshambuliaji wa Barcelona, Luiz Suarez.
Suarez alifunga magoli 31 msimu uliopita akiwa na timu ya Liverpool lakini, magoli matano ya ligi kuu ambayo yamefungwa na Sanchez msimu huu, yamemchanganya mzee Wenger.
Kocha huyo wa Kifaransa, ameeleza kuwa kwa zama hivi bara la Amerika Kusini ndiyo limekuwa tishio katika kuzalisha washambuliaji.
Wenger amesema, miaka ya 1960 hadi 1970, Uingereza pia ilikuwa na washambuliaji mahari kabisa lakini kwa sasa, ukitaka mshambuliaji, nenda Amerika Kusini.
Sanchez ambaye amenunuliwa na kwabu hiyo ya jijini London, msimu uliopita alikuwa na klabu ya Barcelona na kufanikiwa kufunga magoli 19 ya La Liga huku akitengeneza mengine 10.
Wenger ameeleza kuwa, Sanchez anajua kukaba, kufunga na hata kutengeneza magoli kwa wenzie sifa ambazo Luiz Suarez zimemfanya awe juu.
Wenger hakusita pia kutolewa mfano wa timu ya taifa ya Ujerumani ambayo ilitwaa ubingwa wa dunia mwaka huu nchini Brazil huku ikimtegemea mshambuliaji asilia mmoja tu, Miloslav Klose licha ya umri wake kuwa mkubwa (35) .
Wenger amesema, hicho ni kielelezo tosha kuwa, barani Ulaya hakuna washambuliaji bora wengi kwa zama hizi. Ukitazama barani Ulaya kwa sasa, utagundua kuwa zaidi ya alimilia 80 ya washambuliaji wanatoka Amerika Kusini.
0 comments:
Post a Comment