Usiku wa Ulaya umerejea Anfield.
Na Oscar Oscar Jr
Mtaalamu Brendan Rodgers ameendelea kuwa na matumaini makubwa na mshambuliaji wake Super Mario Balotelli kuwa muda si mrefu ataanza kuonyesha makali yake dimbani. Mshambuliaji huyo tayari amecheza mechi mbili akiwa na majogoo hao wa jiji la Liverpool lakini ameshindwa kufunga hata bao moja.
Baada ya kumkosa mshambuliaji mahiri Daniel Sturridge ambaye msimu uliopita alifunga mabao 21 ya ligi kuu, matumaini makubwa kwenye safu ya ushambuliaji yanabakiwa kwa mtaliano Balotelli ambaye licha ya kutofunga kwenye mechi dhidi ya Tottenham na Aston Villa bado alionekana kucheza vizuri.
Kuna kila dalili kwa mshambuliaji huyo kutajwa kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo ambapo Liverpool watawakaribisha mabingwa wa ligi ya Bulgaria timu ya Ludogorets Razgrad kwenye mchezo wa kwanza wa klabu bingwa Ulaya wa kundi B.
Balotelli amecheza Ligi ya mabingwa Ulaya mara 29 na yuko nyuma ya Steven Gerrard (67) na Kolo Toure (62) miongoni mwa wachezaji wa sasa wa Liverpool na amefunga mabao saba. Liverpool leo kwa mara nyingine watajimwaga Anfield baada ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya kwa miaka mitano.
.
0 comments:
Post a Comment