Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 September 2014
Wednesday, September 10, 2014

Kocha Kwesi Appiah siku zake zinahesabika



 Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah anaweza kujikuta kwenye hali ya utata endapo atashindwa kufanya vizuri na kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Togo. 

Mchezo wao dhidi ya Togo una maana kubwa sana kwa Ghana kama wanataka kuweka hai mbio zao za kufuzu kwa AFCON 2015 hapo mwakani.

Ghana walijikuta kwenye hali ngumu mbele ya Uganda kwenye mchezo wao wa kwanza na kulazimishwa kwenda sare ya 1-1 huku wakionyesha upungufu mkubwa sana kwenye safu yao ya kiungo na ushambuliaji. 

Ghana walishindwa kufanya vema mwaka jana kwenye michuano ya AFCON na mwaka huu kwenye kombe la dunia nchini Brazil ambapo waliondolewa kwenye hatua ya makundi.

Taarifa zilizopo ni kwamba FA ya Ghana imeanza kufanya mazungumzo na kocha Milovan Rajevac aliyeiongoza timu hiyo mwaka 2010 kwenye michuano ya kombe la Dunia na kufanikiwa kutinga kwa mara ya kwanza hatua ya robo fainali ili achukuwe mikoba ya kocha mzawa Kwesi Appiah.

 Appiah ana mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka la Ghana ambao uliafikiwa muda mfupi kabla ya Kombe la Dunia. Nahodha huyo wa zamani wa Ghana akitimuliwa, basi GFA watalazimika kumlipa pesa nyingi na kuna tetesi kuwa viongozi wa GFA wako tayari kwa hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!