MAN CITY SASA NI MAJANGA KWA YAYA TOURE
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Manchester City ambao kwa muda mrefu wamepigiwa upatu kushinda taji la Ligi ya Premia, sasa wamejikuta taabani na wana wasiwasi kuhusu hali ya Yaya Toure na Vincent Kompany wiki za mwisho za kampeni yao.
Kushindwa 3-2 na Liverpool katika uwanja wenye hisia wa Anfield, wakati wa maadhimisho ya miaka 25 tangu kutokea mkasa wa Hillsborough, kulipelekea City kuteleza hadi alama saba nyuma ya wenyeji wao mechi hiyo ya Jumamosi na sasa watatarajia klabu hiyo ya Merseyside ijikwae ndipo waifikie.
Mbio za City hadi ushindi wa Kombe la Capital One (League) na robofainali Kombe la FA zilikuwa na maana kwamba miezi michache iliyopita, wamekuwa nyuma kwa alama lakini wakiwa na mechi mbili ambazo hawajacheza wakilinganishwa na wapinzani wao kileleni jambo ambalo limewafanya kuendelea kupigiwa upatu.
Lakini kichapo cha Jumapili kina maana kwamba nafuu yao sasa imepunguzwa na lazima waombe Liverpool washindwe kushinda mechi zote walizosalia nazo dhidi ya Norwich City, Chelsea, Crystal Palace na Newcastle United, hata kama mabingwa hao wa 2012-13 watashinda mechi zote sita walizosalia nazo.
Kichapo Anfield kilitokea baada ya City kupigana kutoka mabao mawili chini na kusawazisha 2-2 kabla ya kuondoa vibaya kwa Kompany kumuwezesha Philippe Coutinho kufunga bao la ushindi kukiwa na dakika 12 zilizosalia za kucheza.
Nahodha huyo wa City aliyewafaa sana alikuwa amepata jeraha baada ya kugongana na Micah Richards mazoezini Jumamosi lakini uamuzi wa kuchezesha difenda huyo wa kati, ulikosa kufana kwani Mbelgiji huyo alishindwa kuwakabili washambuliaji matata wa Liverpool.
Pigo jingine kwa Manchester City lilitokea baada ya dakika 20 pekee pale kiungo wao matata wa kati Toure alipochechemea hadi nje ya uwanja kutokana na jeraha la mtoki, na kuibuwa wasiwasi kwamba huenda raia huyo wa Ivory Coast akakosa mechi ya Jumatano dhidi ya Sunderland na labda kipindi kilichosalia cha msimu.
"Ni vigumu sana kwa Yaya kuwa kwenye mechi yetu ijayo,” meneja Manuel Pellegrini aliambia Sky Sports Jumapili.
"Tutajua hayo kesho, sijui ubaya wa jeraha alilopata. Ninafikiri itakuwa vigumu kwake kucheza hadi mwisho wa msimu huu.”
0 comments:
Post a Comment