KOCHA MARTINEZ KAANZA KUTEMA MKWARA
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Meneja wa Everton Roberto Martinez amewaonya wachezaji wake wasirudi nyuma dhidi ya Sunderland ambao wanahangaika kwa sasa, timu hiyo itakapokuwa ikisaka kumaliza katika nne bora kwenye mechi itakayochezewa Stadium of Light Jumamosi.
Paka hao Weusi wanashika mkia katika jedwali la Ligi ya Premia, alama saba kutoka eneo salama, na wanaoneakana kuwa miongoni mwa watakaoangukiwa na shoka na kupelekwa Championship baada ya kuadhibiwa 5-1 Jumatatu wakiwa mbele ya Tottenham.
Ukiangalia kwa macho, wanaweza kuonekana kuwa wapinzani wazuri kwa Everton walio nambari tano, ambao wanasaka nafasi ya kumaliza katika nne bora na kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Ushindi kwenye dimba la Stadium of Light utawawezesha kupanda juu ya Arsenal ambao kwa sasa ndio wako nambari nne, na ambao walipigwa na Everton 3-0 wikendi iliyopita, lakini hawana mechi ya ligi wikendi hii kutokana na mechi ya nusufainali ya Kombe la FA dhidi ya Wigan.
Hata hivyo, Martinez anaamini kwamba Toffees wataikabili Sunderland ambao wanahisi kwamba hawana presha kwa sababu wamepoteza matumaini ya kunusurika, na hivyo watakuwa wapinzani hatari.
"Huwa unafika mahali katika vita vya kunusurika ambapo huwa huna la kuogopa tena,” Martinez alisema.
"Sunderland wako hapo sasa ambapo wana mechi saba za kucheza na wanazichukulia kwa hali hiyo.
“Wamecheza vyema nyumbani msimu huu – mechi yao dhidi ya Manchester City ikiwa moja. Wanaweza kufanya hayo tena wakati wowote, kama walivyoonyesha katika League Cup ambapo walitisha.
“Itakuwa mechi ya kusisimua sana. Alama zitakuwa na umuhimu sana, na kwa hivyo tunahitaji kujikwamua vyema.
“Mahitaji katika mechi ya Jumapili iliyopita tuliyoshinda 3-0 dhidi ya Arsenal yalikuwa makuu, lakini kiakili klabu yote inahisi vyema na hilo ni jambo ambalo twafaa kulitumia vyema.”
Martinez atamchunguza kiungo wa kati Leon Osman, ambaye alijeruhiwa karibu na jicho lake, huku nahodha Phil Jagielka akikosa mechi hiyo kwani anaendelea kuuguza jeraha la misuli ya paja.
0 comments:
Post a Comment