Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 April 2014
Thursday, April 17, 2014

EVERTON BADO WANAHITAJI NAFASI YA NNE



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858

Meneja wa Everton Roberto Martinez ana imani kwamba klabu yake inaweza kumaliza nambari nne kwenye Ligi ya Premia licha ya kupokezwa kichapo cha “kuumiza” cha 3-2 na Crystal Palace uwanjani Goodison Park Jumatano. 

Baada ya kushinda mechi zao saba zilizopita za ligi, imani ya Everton ilikuwa juu, lakini walishindwa kutamba mbele ya Palace wanaonolewa na Tony Pulis na matokeo hayo yaliwaacha nambari tano kwenye msimamo huku wakiwa na alama 66 kutokana na mechi 34. 

“Tunasikitika sana,” Martinez aliwaambia wanahabari.
“Matokeo hayo yanaumiza kwa sababu ya matarajio ambayo tulikuwa nayo na hamu ambayo tulikuwa nayo tukiingia kwenye mechi hii.” 

Kukiwa na mechi nne zilizosalia, Everton wako nyuma ya Arsenal walio nambari nne kwa alama moja lakini wana mabao mengi.
Licha ya mechi ngumu zijazo dhidi ya Manchester City na Manchester United, Martinez anaamini timu yake inaweza kumaliza miongoni mwa nne za kwanza kwa mara ya kwanza tangu 2005. 

"Tuna mechi 12 za kuchezea, tuko karibu na nambari nne na bado tuko katika nafasi nzuri,” alisema.
"Sifikiri Arsenal watachukua alama zote kutoka kwa mechi zilizosalia. 

“Baada ya wikendi (kuondolewa kwenye nne bora) ni jambo la kusikitisha, lakini ukiangalia msimu ulivyokuwa, ni nafasi nzuri.”
Mabao ya Jason Puncheon na Scott Dann yaliwaweka Palace 2-0 mbele Goodison Park kabla ya nguvu mpya Steven Naismith kufanikiwa kuchomoa bao  moja kwa upande wa Everton. 

Bao la Cameron Jerome lilirejesha uongozi wa mabao mawili wa Palace na licha ya bao la dakika za mwisho lake Kevin Mirallas, Martinez aliachwa akijutia uchezaji mbaya wa timu yake kipindi cha kwanza. 

“Kipindi cha kwanza tulicheza vibaya sana kiasi kwamba tulisahau mambo ya kawaida,” akaongeza Mhispania huyo.
“Kipindi cha pili, mambo yalikuwa tofauti kabisa. Tulicheza vyema na kurudia hali yetu halisi. 

"Nilihisi kwamba tulikuwa na mkosi kiasi cha kutopata sare kutokana na nafasi tulizotengeneza.”
“Jinsi tulivyomaliza kipindi cha pili inanipa matumaini kwamba tunaweza kumaliza msimu vyema.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!