TIM KRUL NJE WIKI MBILI AU TATU.
Kipa Mholanzi anayechezea Newcastle United Tim Krul atakaa nje wiki mbili au tatu kutokana na jeraha la goti, meneja Alan Pardew alisema Alhamisi.
Krul, ambaye anataraji kuitwa kwenye kikosi cha Uholanzi cha Kombe la Dunia, alijeruhi goti lake wakati wa mechi iliyomalizika kwa kichapo cha 3-0 Ligi ya Premia dhidi ya Everton Jumanne.
"Tim hatacheza (dhidi ya Southampton wikendi)," Pardew, ambaye bado anatumikia adhabu ya kutokuwa uwanjani, alisema.
"Atakuwa nje kwa mechi mbili au tatu zijazo bila shaka, kwa hivyo Rob Elliot ndiye atacheza.
" (Elliot) Amefanikiwa kuitwa timu ya taifa lake, anataka kukaa kwenye kikosi hicho. Anahitaji kucheza na hivyo nafasi imemwangukia.
“Rob ni kipa mwenye kujiamini, na atajizatiti na kufana.”
0 comments:
Post a Comment