Meneja wa Chelsea Jose Mourinho, amesema anaamini straika Mario Balotelli
ataendelea kubaki kuwa mchezaji wa AC Milan na kwamba hafikirii hata
chembe mpango wa kumsajili Mtaliano huyo kwa sababu si mchezaji
anayemhitaji.
Staa huyo mwenye vituko vingi ndani na nje ya
uwanja, kwa siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua
Stamford Bridge mahali ambapo Mourinho ni kocha mkuu.
Mourinho alisema anaamini Balotelli ataendelea
kuichezea AC Milan, licha ya kwamba klabu hiyo kwa sasa mambo hayaiendei
vizuri kwenye Ligi Kuu Italia.
Mourinho ambaye aliwahi kumnoa Balotelli
walipokuwa pamoja katika klabu ya Inter Milan, alisema: “Mario anacheza
kwenye moja ya klabu maarufu duniani.
“Clarence Seedorf (kocha wa AC Milan), naye
anamhitaji sana, anahitaji muda pia na kutulia na wachezaji kama
Balotelli. Naamini maisha ya Mario yataendelea kubaki Milan.”
Balotelli amefunga mabao 27 kwenye mechi 44 alizocheza tangu alipohama Manchester City mwanzoni mwa mwaka 2013.
0 comments:
Post a Comment