Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

LIVERPOOL MWENDO MDUNDO MPAKA KIELEWEKE.



Brendan Rodgers ameendelea kusisitiza kuwa kumekuwa hakuna  mjadala juu ya Liverpool na uwezekano wa kutwaa taji la ligi kuu na hali hiyo inawakumba Chelsea na kuzidi kuwapa presha na shinikizo la kutwaa taji hilo kutoka kwa viongozi wa klabu.Liverpool itasafiri kuwafuata Cardiff siku ya Jumamosi ikiwa pointi nne nyuma ya vinara  Chelsea, na mchezo mmoja mkononi na kwa upande wa Jose Mourinho bado hajakutana na wababe hao wa  Anfield kwa mara ya pili.

Ushindi walioupata Liverpool mwishoni mwa wiki iliyopita wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United umewafanya waweza kujikusanyia alama 26 kati ya 30 tangu kuanza kwa mwaka 2014 na kufufua matumaini ya kuweza kutwaa taji la ligi ambapo mara ya mwisho,Liverpool walitwaa mwaka 1990. 


Baada ya safari ya Wales, kikosi cha Liverpool wataumana na wachovu Sunderland na watu wanaochechemea ,timu ya Tottenham kabla ya kusafiri kwenda kumenyana na timu ya West Ham.Michezo ya nyumbani itakayofuata itakuwa dhidi ya Manchester City na Chelsea na,kwa upande wa ugenini,itakuwa ni safari ya Norwich na kumaliza kampeni na mechi dhidi ya Crystal Palace na Newcastle.


Lakini meneja wa Liverpool Rodgers amesema bado ni ngumu kupata ubingwa na  hata ushindi muhimu katika dimba la Old Trafford amekuwa na wachezaji wake wakijadili namna ya kuendelea kupata matokeo bora na kukomesha ukame katika klabu hiyo ya  Anfield.


" Haya yalikuwa ni matokeo ya ajabu katika dimba la Old Trafford lakini hakuna majadiliano juu ya Ubingwa. Sisi ni kufurahia tu kazi yetu na kulenga mechi yetu dhidi ya Cardiff."Mimi sijui jinsi kupata fursa nzuri ya kushinda taji la ligi. Kuna mchezo mgumu mbele yetu,ni mchezo mgumu dhidi ya Cardiff. Sisi tutazungumzia kuhusu Ubingwa mwishoni mwa msimu ."Kiungo fundi wa wales Joe Allen wa Liverpool ufanisi wake umekuwa mndogo msimu huu kutokana na kuumia na aina ya watu wengine kwenye timu walivyoongezeka ubora.

 
Meneja wa timu ya Cardiff city,Ole Gunnar Solskjaer ameshindwa kuboresha matokeo ya mtangulizi wake, Malky Mackay, na wafuasi wa Cardiff wana mipango ya maandamano dhidi ya mmiliki Vincent Tan kabla ya mechi.

 
Liverpool itakuwa na lengo la kutumia faida kamili ya matatizo ya wenyeji wao na kujipatia ushindi.Mshambuliaji Craig Bellamy wa Cardiff city , aliyekuwa nguzo ya Anfield siku za nyuma mwenyewe amesema: "Hii timu ya Liverpool ya sasa, ndiyo  timu ambayo mimi nilikuwa naifahamu.wako juu kwa sasa .

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!