Wakati Roman Abramovich alipoinunua Chelsea kutoka kwa Ken Bates miaka 10 iliyopita, hakuna aliyeweza kutabiri namna ambavyo mrusi huyu angeweza kuitingisha Premier League.
Huku akiwa ameona Manchester United ikitawala soka la kiingereza tangu kuanzishwa kwa premier league, The Blues ghafla wakawa moja ya timu zilizoanza kutishia utawala wa United baada ya utawala wa Abramovich kuanza kazi.Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, billionea huyu wa kirusi alitoa kiasi cha £150million za usajili - akiwaleta wachezaji kama Hernan Crespo, Claude Makelele na Juan Sebastian Veron Stamford Bridge.
5) Juan Mata
Wakati akiwa mmoja wa wachezaji wapya kuwasili darajani, mhispani huyu ndio anayetoa sura ya mbele ya klabu ya Chelsea.Juan Mata aliwasili akitokea Valencia kwa ada ya uhamisho wa £23.5m August 2011 na alipewa tuzo ya mchezaji wa mwaka wa klabu baada ya kuisadia timu ya Roberto Di Matteo iliyoshinda ubingwa wa FA Cup na Kombe la mabingwa wa ulaya.
Kijana huyu anatajwa kuwa Gianfranco Zola, msimu uliopita aliiongoza Chelsea kushinda ubingwa wao wa kwanza Europa League. Japokuwa anatajwa kuwa anaweza kuuzwa za Mourinho darajani.
0 comments:
Post a Comment