Rais
Jakaya Kikwete Mgeni Rasmi Mechi ya hisani itakayowakutanisha
waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na
Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini
Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya
albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na
wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya
wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila
wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi
yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake. Alisema
kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo
wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa
wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya
wabunge.
“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu
kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku
barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika
kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
“Katika mechi hizi,
mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa
Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na
Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa
ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman
Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus
Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba),
Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu
(Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah
Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin
Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe),
Muhingo Rweyemamu (handeni), Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima
(Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea),
Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni,
ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.
Aidha, Muhingo alitaja
kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba
(Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni
Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina
Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna
Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).
0 comments:
Post a Comment