Timu
ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inaingia dimbani leo mjini Marakech
Morocco kukwaana vikali na timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Simba
wa Atlas katika kuwania tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia huko
Brazil 2014.
Timu hizo zinakutana huku kukiwa na kumbukumbu ya
ushindi mzito wa Taifa Stars wa 3 - 1 dhidi ya Morocco jijini
Dar-es-salaam mwezi March mwaka huu.
Kocha wa Morocco, Rachid
Taoussi atawatumia mastaa wake Youssef el Arabi, Adil Hermach, Youness
Belhanda na Abderrazak Hamdallah kuitikisa ngome ya Tanzania ambayo nayo
itawategemea sana wakali wake wakiongozwa na kipa Juma Kaseja, Mrisho
Ngassa, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta. Taifa Stars iko nyuma ya Ivory Coast kwenye kundi D, huku Morocco ikifuata kwenye nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment