SIMBA WANAONA MBALI
Simba sc kuna vitu vingi ambavyo wananifurahisha kwanza,ni swala la wao kujikita zaidi kuibua na kuinua watoto wa Tanzania katika soka.Wameweza kuwatambulisha vijana wengi tu kama SINGANO n.k.Wameamua kuijenga timu yao katika misingi ya vijana ambao wengi ni wazawa wa Tanzania,nadhani hiki ni kitu kizuri ambacho baadae kitasaida kutupa wachezaji wengi bora na wenye uzoefu kwenye timu yetu ya Taifa.
Msimu ujao watakuwa wamezidi kwenda mbele baada ya kuamua kumpa mikoba ya ukocha ABDALLA KIBADENI huku akisaidiwa na JULIO.Hawa ni watu sahihi kwa simba kwasababu kwanza wanajua mazingira yote ya Club ya simba na utamaduni wake na mashabiki wao.Wamefanya kazi na makocha wengi wa kigeni na kupata uzoefu na mbinu,nadhani simba itakuja kuwa tishio kama hawa watu watapewa huduma kama zile wanazopewa makocha wageni na kuachiwa wao wafanye kazi yao bila kuingiliwa na mtu.
Makocha wa kigeni sio wabaya kuja Tanzania kwa sababu bado tunawahitaji ili tuweze kujifunza mengi kutoka kwao ila kama tuna watu wazawa ambao wanaweza kufanya kama ambacho wageni hao wanafanya ni bora tukawapa wazawa nafasi ili kuwajengea imani na uwezo.Mimi naamini wazawa wanaweza,tuwape nafasi.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.