Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 June 2013
Sunday, June 02, 2013

NIGERIA NA KENYA WAINGIA UTATA KUFUZU BRAZIL 2014

George Opiyo Otieno
Chama cha soka nchini Kenya FKF kimelaumu chama cha soka cha Nigeria FA,kwani hadi sasa chama cha soka hapa Kenya haijapata mawasiliano yeyote kutoka Nigeria.
Sheria ya FIFA yakufuzu kwenye kombe la dunia huko BRAZIL,kurasa ya 19 aya ya 2 inasema wazi kwamba,nchi inayosafiri inafaa ifahamishe nchi mwenyeji,tarehe,saa na idadi ya wageni mwezi mmoja kabla ya mechi.

Hii inaonyesha wazi kwamba tayari Nigeria imevunja sheria ya FIFA lawama hizi zilitolewa kwenye vyombo vya habari na katibu mkuu wa FKF Bwana Michael Esakwa.
Nigeria inaogoza kundi hilo kwa alama tano,wakati Kenya inavuta mkia ikiwa na alama 2.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!