KLABU
ya Cardiff City imejitoa kwenye mbio za kuwania saini ya Victor Wanyama
baada ya klabu yake, Celtic kushindwa kuidhinisha ofa waliyotoa kwa
ajili ya kiungo huyo.
Kocha
wa Cardiff, Malky Mackay bado anamtaka sana Mkenya huyo na amepandisha
ofa yake baada ya ile awali ya Pauni Milioni 10 kukataliwa na Peter
Lawwell Jumatatu.
Celtic
tayari imekubali Pauni Milioni 12 kutoka Southampton wiki iliyopita,
lakini mawakala wa kiungo huyo, Rob Moore na Ivan Modia, wamekataa
kutokana na kutoridhishwa na vipengele vya maslahi binafsi ya mchezaji.
Mtu anayetakiwa: Kiungo wa Celtic, Victor Wanyama (katikati) anayetakiwa na Cardiff
BIN
ZUBEIRY inafahamu Cardiff imekwishafikia makubaliano na wawakilishi wa
Wanyama juu ya mshahara anaotaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
Sasa klabu hiyo ya Parkhead lazima iamue aidha kutoa fursa ya mazungumzo rasmi kuanza — na Cardiff inajiandaa kupanda dau.
Kocha
wa Celtic, Neil Lennon anaamini kiungo huyo amekwishacheza mechi yake
ya mwisho katika klabu hiyo, na anaamini mchezaji huyo ataondoka wakati
wowote.
Kumbuka jina hilo: Wanyama anaonekana anataka kuhamia Celtic akacheze Ligi Kuu ya England
0 comments:
Post a Comment